제1단계 3차년도 현지조사(양철준)

양철준1-3(Ukerewe)

양철준 HK연구교수는 1단계 2차년도 연구의 연장선상에서 2013년 7월 10일부터 8월 1일까지 탄자니아의 우케레웨에서 현지조사를 실시했다. ‘케레웨인들의 언어 유지와 교체: 종족어의 활력에 영향을 미치는 요소들(Language maintenance and shift among the Kerewe: Factors contributing to ethnolinguistic vitality)’을 주제로 삼아, 아래와 같이 표준화된 설문지를 사용하여 우케레웨 섬에 소재하고 있는 초중등학교에 재학 중인 학생들을 대상으로 설문조사를 행했다. 연구 결과는『아프리카 사회의 지형, 그 경계 넘나들기』(2014년, 다해, 15-76)라는 제목의 공저에 수록되었다.

Questionnaire

  1. Umri:

Jinsia:

Darasa/kidato:

Mahali ulipozaliwa(Mkoa)………………..(Wilaya)…………………(Kata)………………….

Mahali ulipokaa(Mkoa)………………..(Wilaya)…………………(Kata)……………………..

Dini:

  1. Lugha ya baba:

Lugha ya mama:

  1. Kabila lako (Kiutamaduni na kijamii unajitambulisha kama mtu wa kabila gani?)
  2. Ujuzi wa lugha (lugha unazoweza kutumia)
Lugha Kusikiliza Kuzungumza Kusoma Kuandika
Kikerewe/Ekikerebe
Kiswahili/Ekiswahili
Kiingereza
Kijita/Echijita
Nyinginezo (taja 1)

Kigezo: 1: Vizuri (kwa ufasaha)

2: Wastani

3: Kidogo

  1. Lugha gani hupendelewa kutumiwa katika mazungumzo ya kimsingi katika hali zifuatazo za mazungumzo.
  2. i) Unapozungumza na wazazi wako nyumbani mnaongeleshana kwa lugha g gani?
  3. ii) Unapozungumza na babu na bibi yako

– Wanakuongelesha kwa lugha gani?

– Unawaongelesha kwa lugha gani?

iii) Unapozungumza na marafiki zako nje ya darasa/shule

  1. iv) Unaposalimiana na mwanakijiji mwenzako
  2. v) Unapokutana na mgeni katika kijiji chako
  3. vi) Mkutano wa hadhara unapofanyika katika kijiji (kikao cha kijiji)

vii) Uingiapo kwenye ofisi za kiserikali, hospitali, zahanati au mahakama

viii) Ununuapo vitu dukani/sokoni

  1. ix) Kunapokuwa na mkutano wa jamaa kwa kujadiliana kuhusu harusi/ndoa au msiba
  2. Kwa maoni yako Kikerewe cha mahali gani (mjini au kijijini) kingechukuliwa

kuwa Kikerewe safi na sanifu (Taja jina la mahali hapo)

  1. Unajivunia lugha yako ya mama, yaani Kikerewe?
  2. Inawezekana kubaki Mkerewe bila kuongea Kikerewe?
  3. Ni lazima uongee Kikerewe ili kutambuliwawa kuwa Mkerewe?
  4. Kikerewe kinastahili kufundishwa katika mazingira rasmi kama vile mfumo wa elimu?
  5. Unataka Kikerewe kirithishwe kwa Wakerewe wa kizazi cha sasa na wa kijacho?
  6. Nini ifanyike kudumisha uhai na matumizi ya Kikerewe?
  7. Unataka serikali itimize (ifanye) nini kwa kustawisha Kikerewe na kwa kuhamasisha Wakerewe kuendeleza lugha yao ya mama?
  8. Kwa nini unapenda kutumia Kikerewe (lugha mama) kama lugha ya mawasiliano wakati Kiswahili kipo?
  9. Unapotumia lugha ya Kiswahili katika jamii uliyopo (inayokuzunguka) unaelewekaje?
  10. Je, baada ya kuingiza Kiswahili kiwe lugha ya kufundishia kwa elimu ya msingi kitakuwa kimeathiri mila na tamaduni za kikabila?
  11. Lugha ya Kiswahili inatumika zaidi katika maeneo/mazingira yapi zaidi katika jamii uliyopo?
  12. Je, lugha ya Kiswahili inatumika zaidi katika watu wa rika lipi?
  13. Kwa nini lugha ya Kiswahili inakua zaidi katika rika hilo?
  14. Lugha ya Kiswahili inapoendelea kukua katika rika la vijana inakuwa inasababisha kupotea kwa lugha mama?
  15. Mara kwa mara unakuta maneno magumu (yanayokutatanisha) ya Kiswahili au Kiingereza ambayo yangekuwa rahisi zaidi iwapo yanaelezwa kwa Kikerewe?
  16. Unapokutana na Mjita, lugha ipi kati ya Kikerewe na Kijita inapendelewa? Eleza sababu zake.
  17. Unapobadilisha chaguo la lugha kutoka lugha moja hadi nyingine ubadilishaji huo unasababishwa:
  18. i) Kwa lengo gani?
  19. ii) Katika hali gani?
  20. Lugha gani zipewe kipaumbele (umuhimu) kwa siku za usoni katika maisha yako?